LOVESTORY MOVIES🔞 WAKUBWA TU

Ingia Hapa

Thibitisha Umri Wako

Je wewe ni mpenzi wa simulizi?

Hii ni kwawadau wanaopenda kusoma simulizi bonyeza button hiyo juu kisha chagua aina ya simulizi..

KARIBU KWA HUDUMA KAMA | GRAPHICS DESIGNER | MOVIES NA SERIES FULL HD | HUDUMA ZA MTANDAONI | VIFAA VYA COMPUTER NA MATENGENEZO | VIFAA VYA SIMU NA MATENGENEZO | KUTENGENEZEWA WEBSITE/BLOGS | WASILIANA NASI KUPITIA LIVE CHATI HAPO CHINI AMA TUPIGIE SIMU YA OFISI 0262605123

KAA KARIBU NASI KWA KUJIUNGA KATIKA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPO CHINI

KWA WATEJA WETU WA MBALI LIPIA HUDUMA HAPA NA THIBITISHA MALIPO YAKO NASI TUKUHUDUMIE KWA UAMINIFU MKUBWA
📱JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP

TANGAZA HAPA 🎉CHEZA USHINDE ZAWADI💰

DAMU YA KIFAMILIA

RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA
MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
MWAKA: 2024/2025
SMS & WHATSAPP*: *0752474397

UTANGULIZI
Kila familia ina siri zake lakini si kila siri inabaki kufichika milele. Katika maisha, matukio tunayoyapuuzia mara nyingi huwa chemchemi ya matatizo makubwa yanayokuja

Hii ni simulizi ya familia moja, familia iliyoficha historia ya damu, chuki na uhasama wa vizazi lakini kila kizazi kina jukumu la kulipa madeni ya dhambi za waliowatangulia

Safari ya familia ya Karungi inatufundisha kuwa ukimya si suluhisho na kwamba giza la ndani ya nafsi linaweza kuligharimu taifa zima

Soma ukiwa tayari kutafakari, kuguswa na kutetemeka

*SEHEMU YA KWANZA*

Kijiji cha Mwikambe kilikuwa kimya, utulivu uliovurugwa tu na milio ya upepo mkali uliovuma kupitia mapengo ya nyumba za udongo. Familia ya Mzee Karungi ilikuwa imejikusanya ndani ya nyumba yao ndogo, kila mmoja akiwa na mawazo mazito. Jua lilikuwa limezama na giza lilianza kufunika anga la kijiji hicho maskini

Mzee Karungi alikaa kimya kwenye kigoda chake cha zamani, mikono yake iliyochoka ikiwa imeshika shavu lake. Macho yake yalikuwa yameelekezwa kwa binti yake wa mwisho Neema, aliyekuwa amelala chini ya blanketi lililochakaa, uso wake ukionekana kuwa wa maumivu makubwa

Zawadi mke wa Karungi alijitahidi kumchangamsha mumewe

"Karungi, mtoto wetu anaendelea kudhoofika na hatufanyi chochote cha kumsaidia. Umaskini huu unazidi kuwa mzigo"

Karungi alikohoa kidogo akitafuta maneno ya kumfariji mke wake

"Kesho nitampeleka kwa mzee Mbalamwezi, mganga wa jadi lazima tujaribu kila njia. Mungu atatuonyesha njia"

Neema aligeuka kwa tabu na kufumbua macho

"Baba... mama... kuna watu wananiita usiku wananiambia nifuate njia ya mto mkubwa. Nawaona wakinijia... uso wao ni wa kutisha"

Maneno yake yaligubika chumba kwa hofu. Baraka, kaka mkubwa wa Neema mwenye umri wa miaka 16, alisimama haraka

"Baba, haya maneno si ya kawaida kuna kitu kibaya kinachotokea hapa"

Karungi alimtazama mwanae kwa macho ya tahadhari

"Tulia Baraka hatuwezi fanya uamuzi wa haraka tunahitaji msaada"

Baada ya chakula cha jioni cha ugali na mboga za kunde, familia ilijitayarisha kulala. Zawadi alimuombea Neema kwa sauti ya chini, akimfunika vizuri na blanketi. Karungi alikaa macho kwa muda mrefu akili ake ikiwa imejawa na mawazo yasiyoisha

Ilikuwa karibu saa sita usiku wakati kilio cha ajabu kilipoanza kusikika nje. Ilianza kwa sauti ya chini kisha ikazidi kuwa kubwa kuna mtu alikuwa akilia kwa uchungu mkubwa

"Unasikia hiyo?"

Zawadi aliuliza kwa hofu akimshika Karungi kwa bega

Karungi alisimama akashika rungu lake dogo na kuelekea mlangoni kwa tahadhari

"Endelea kukaa na watoto nitachunguza"

Alipofungua mlango kidogo upepo mkali ulivuma ndani ya nyumba alitazama nje kwa makini lakini hakukuwa na kitu cha kawaida. Kilio kilikuwa kimetulia lakini mara aliposogea mbele zaidi, sauti ndogo ilisikika karibu nae

"Karungi... umesahau huwezi kuficha milele"

Karungi alishtuka na kurudi ndani kwa haraka akikaza mlango kwa mkono wake wa nguvu. Alipomgeukia Zawadi hakuweza kusema neno lakini macho ake yalitoa ujumbe wa hofu kuu

Asubuhi iliyofuata Karungi alimpeleka Neema kwa mganga wa jadi mzee Mbalamwezi. Nyumba ya mganga ilikuwa imezungukwa na miti mikubwa yenye majani yaliyokauka na harufu ya dawa za asili ilijaza hewa

Mbalamwezi alimwangalia Neema kwa makini kisha akaanza kuzungumza kwa sauti nzito

"Huyu mtoto hana ugonjwa wa kawaida kuna damu inayolilia haki, familia ako imebeba mzigo wa giza wa vizazi kama hautachukua hatua sasa laana hii itamaliza kizazi chako"

Karungi alitetemeka..

"Mzee ni nini unachomaanisha...ni laana gani hii?"

Mbalamwezi alimpatia hirizi ndogo ya shanga na kusema..

"Hii itamlinda kwa muda mfupi lakini huwezi kukwepa ukweli.. Laana hii ilianza zamani na chanzo chake ni damu iliyomwagika bila haki"

Maneno ya mganga yalimrudisha Karungi kwenye tukio la zamani ambalo alikuwa amelificha kwa muda mrefu

Miaka 20 iliyopita Karungi na kaka yake mkubwa Kirama, waligombana kuhusu urithi wa shamba la familia. Katika hasira zake, Karungi alimshambulia Kirama ambae baadae alikufa kwa njia isiyoeleweka. Hakuna aliyejua ukweli lakini Karungi alijua dhambi hiyo ilikuwa juu yake

Siku ya mazishi mama yao aliapa..

"Familia hii haitapata amani hadi damu ya haki itakapomwagika tena"

Karungi alirudi nyumbani akiwa na hirizi ya mganga lakini hakuwa na utulivu, akili ake ilikuwa ikipambana na kumbukumbu za zamani na maneno ya mganga

Alipokuwa akifunga mlango wa nyumba yake, upepo mkali ulianza kuvuma tena kisha sauti nyembamba ya ajabu, ikasikika karibu nae..

"Karungi...siri zako hazitakaa zikufiche milele...

USIKOSE SEHEMU YA PILI

Je, Karungi atakabiliana na ukweli wa dhambi zake au familia yake itaendelea kusumbuliwa na giza la laana ya kifamilia?

[12/12, 10:15 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA: 2024/2025*
*SMS & WHATSAPP*: *0752474397*

*SEHEMU YA PILI*

*ILIPOISHIA*

"Karungi...siri zako hazitakaa zikufiche milele"

Maneno hayo yaliugubika moyo wa Karungi kwa hofu, aligeuka haraka lakini hakukuwa na mtu yeyote. Upepo ulivuma kwa nguvu ukisababisha kelele za mapaa ya nyasi kusikika kama yalikuwa yanalia

Alirudi ndani kwa mwendo wa haraka akiufunga mlango kwa nguvu na kusukuma kigoda mbele yake kama kinga

Zawadi akiwa na wasiwasi mwingi aliuliza kwa sauti ya chini..

"Karungi nini tena"
Karungi alikataa kujibu badala ake akaketi kimya huku akimtazama Neema aliyekuwa amelala chini lakini akili yake ilikuwa ikisikia maneno ya mganga wa jadi Mbalamwezi kama kengele inayolia mara kwa mara ikisema *“Kuna damu inayolilia haki”*

*************************

Usiku huo usingizi ulikuwa ndoto kwa Karungi, alisikia kelele zisizoeleweka kila alipofumba macho na kila mara alihisi kuna macho yaliyokuwa yakimchunguza kutoka gizani

Hatimae aliamua ilikuwa lazima afanye jambo kulinda familia ake

Asubuhi aliwaita Zawadi na Baraka

"Tunapaswa kurudi kwa Mbalamwezi" alisema kwa sauti nzito..."Lazima tujue zaidi kuhusu hii laana..lazima tujue jinsi ya kuikomesha"

Baraka ambae alikuwa jasiri kuliko miaka yake, alimuangalia baba yake moja kwa moja machoni

"Baba inaonekana kuna kitu unachokijua lakini hutaki kusema. Hii sio mara ya kwanza kusikia mambo haya. Unaogopa nini"

Karungi hakujibu mara moja. Macho ake yalielekea chini.. moyo wake ukimtwanga kwa hofu na majuto

"Baraka... kuna mambo ambayo si rahisi kuelezea ila nakuahidi nitakuhifadhi wewe na dada ako kwa gharama yoyote"

Safari ya kurudi kwa Mbalamwezi ilikuwa ya kimya...njia ya porini ilijaa miibana upepo wa asubuhi ulikuwa mkali na wa baridi

Neema aliyekuwa dhaifu zaidi alibebwa na Baraka. Wakati walipofika kwa Mbalamwezi, mganga aliwasubiri nje ya kibanda chake lakini alijua watakuja

Mbalamwezi aliwakaribisha kwa ishara ya mkono..

"Karungi... wewe ndie unayeshikilia majibu ya mateso ya familia yako. Ukitaka kuikomboa familia yako lazima ukiri ukweli, laana haiwezi kuondolewa kwa ukimya"

Baraka aliinamisha kichwa akikaza meno yake..

"Baba tunahitaji kujua...ni ukweli gani unaficha?"

Karungi aliyekuwa akitetemekaalianza kusimulia kisa cha miaka 20 iliyopita. Alieleza ugomvi wake na Kirama jinsi alivyomsukuma kwa hasira na matokeo ya kifo chake

"Sikutaka afe" alisema kwa sauti iliyojawa na maumivu..."Nilihofia kusema ukweli, niliishi kwa hofu, lakini sasa naona imekuwa mzigo kwa nyinyi wote"

Maneno yake yaligubika hema la mganga kwa ukimya mzito, Mbalamwezi alimuangalia Karungi kwa macho makali

"Dhambi yako imeunda giza kubwa juu ya familia yako..Ili kuondoa laana hii, lazima utafute mzawa wa Kirama...ni lazima uombe msamaha kwa dhati na lazima damu ya mnyama safi itolewe kama sadaka ya utakaso"

Karungi alilia machozi ya majuto huku akijua kuwa safari yake ya kumtafuta mzawa wa kaka yake sio rahisi. Alikuwa tayari kujitolea vyovyote ili kuokoa familia yake

Lakini je, msamaha unaweza kuja kirahisi? Je, damu ya sadaka inaweza kuosha dhambi ya damu iliyomwagika?

Mbalamwezi alimpatia Karungi kifurushi kidogo cha dawa na kusema

"Hii itakusaidia kwa muda lakini kumbuka muda unayoyoma"

*USIKOSE SEHEMU YA 3*
[12/12, 10:15 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA: 2024/2025*

*SEHEMU YA TATU*

*ILIPOISHIA*

"Hii itakusaidia kwa muda lakini kumbuka muda unayoyoma"

Maneno ya mzee Mbalamwezi yalizidi kumtesa Karungi hata baada ya kurejea nyumbani. Familia yake hasa Neema ilikuwa ikizidi kudhoofika na alifahamu kuwa kusubiri zaidi kulihatarisha maisha yao lakini safari ya kutafuta mzawa wa kaka yake, Kirama haikuwa rahisi

Karungi alikusanya ujasiri wake na kuanza safari, aliingia chumbani kwake na kufungua kisanduku cha zamani kilichofichwa chini ya kitanda. Ndani yake kulikuwa na barua za miaka mingi iliyopita pamoja na nyaraka za familia...alivuta moja ya barua za Kirama macho yake yakitua kwenye sentensi moja..

*"Kama lolote litazuka, mtafute mtoto wangu wa pekee anaitwa Baruti atakuwa ndie mwokozi wa familia*"

Karungi alikumbuka kuwa Barutii alikuwa amehamia kijiji cha Ng’omongo miaka mingi iliyopita baada ya kifo cha baba ake

Hakujua hali yake ya maisha lakini sasa hakukuwa na njia nyingine aliamini kwamba Baruti ndie ufunguo wa kuvunja laana ya kifamilia

Safari ya Ng’omongo haikuwa rahisi, njia zilikuwa zimejaa vumbi na upepo wa jua kali ulifanya kila hatua kuwa nzito. Karungi alikuwa amebeba hirizi ya mzee Mbalamwezi ambayo aliambiwa itamkinga dhidi ya roho za kisasi

Alipofika kijijini watu walimkazia macho kwa mshangao maana hakuwa mgeni wa kawaida. Alianza kuulizia kuhusu Baruti lakini kila mtu aliyemuuliza alionekana kusita. Mwishowe mzee mmoja aliyevalia shati chakavu alimwambia..

"Baruti....Alikuwa hapa miaka mingi iliyopita lakini alihama ghafla baada ya matatizo na familia yake ya kambo. Sikumbuki wapi alikokwenda"

Karungi alihisi hofu ikimkaba koo...kama Baruti hapatikani, familia ake ilikuwa imehukumiwa lakini mzee huyo alimpa dalili kidogo..

"Unaweza kujaribu kumtafuta kwenye kijiji cha jirani, Kyela. Nasikia alijaribu kuanzisha maisha mapya huko"

************************

Karungi alijikuta akipambana na mawazo mengi njiani. Je, Barutii atakubali kumsamehe...na atawezaje kueleza uhalifu alioufanya dhidi ya baba yake?

Hata hivyo moyo wake ulijawa na matumaini kwamba huu ungekuwa mwanzo mpya kwa familia ake

Alipofika Kyela, aligonga mlango wa nyumba moja iliyokuwa imejificha kwenye msitu mdogo. Mwanaume mrefu aliyeonekana kuwa na umri wa miaka thelathini alitoka nje. Macho yake yalikutana na ya Karungi kwa muda mfupi kabla ya kusema kwa sauti nzito..

"Karungi... wewe ni nani na unatafuta nini hapa"

Karungi alimeza mate akijitahidi kukusanya maneno...

"Baruti... mimi ni mjomba wako...nina jambo zito la kukuambia. Tafadhali nipe muda wako"

Baruti alisita kisha akafungua mlango kikamilifu..

"Ingia lakini ujue sijawahi kusikia chochote kizuri kuhusu ukoo wako"

Karungi aliketi kwenye kigoda na kuanza kueleza, alimueleza Baruti kuhusu giza lililoikumba familia yao, kifo cha Kirama na laana iliyoanza kuathiri kizazi chao. Alimaliza kwa kusema..

"Baruti naomba msamaha kwa dhambi zangu lakini zaidi ya yote naomba msaada wako ili kulinda kizazi chetu... Bila wewe, Neema na familia yetu nzima wamo hatarini"

Baruti alitazama nje ya dirisha kwa muda mrefu...

"Karungi uliniangusha mara moja kwa kumfanyia baba yangu dhambi kubwa lakini siwezi kuangalia familia yetu ikiteketea. Nitakusaidia lakini unapaswa kuelewa kuwa safari hii itahitaji ujasiri na dhabihu kubwa"

Karungi na Baruti walikubaliana kurudi Mwikambe kwa maandalizi ya ibada ya kuvunja laana lakini bila wao kujua, roho za kisasi zilikuwa zikifuatilia kila hatua yao zikisubiri fursa ya kushambulia...

*USIKOSE SEHEMU YA 4*

*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*0752474397*
[12/12, 10:16 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA: 2024/2025*

*SEHEMU YA NNE*

*ILIPOISHIA*

Karungi na Baruti walikubaliana kurudi Mwikambe kwa maandalizi ya ibada ya kuvunja laana lakini bila wao kujua, roho za kisasi zilikuwa zikifuatilia kila hatua yao zikisubiri fursa ya kushambulia

Safari ya kurejea Mwikambe ilikuwa ngumu na iliyojaa ukimya mzito, kila mmoja alikuwa amezama katika mawazo yake akifikiria hatma ya familia yao

Walifika nyumbani usiku wa manane wakiwa wamechoka lakini wenye matumaini ya kuwa pamoja wangeweza kufanikisha mpango huo

Mzee Mbalamwezi alikuwa akisubiri nje ya nyumba ya familia akiwa na hirizi na vifaa vya kutekeleza ibada. Alimtazama Baruti kwa macho makali yaliyojaa udadisi

"Huyu ndie mtoto wa Kirama" aliuliza kwa sauti nzito

"Ndio" Karungi alijibu huku akimwangalia Baruti kwa matumaini

Mzee huyo alitikisa kichwa taratibu akionekana kuridhika..

"Basi tumejiandaa kwa usiku wa giza kuu..hii ndio siku pekee tunapoweza kukabiliana na laana hii"

Familia nzima ilikusanyika kwenye uwanja wa nyumba hiyo ikiongozwa na mzee Mbalamwezi. Baruti alihisi mzigo wa jukumu lake ukiwa mkubwa zaidi kila dakika ilivyozidi kupita

Mbalamwezi alichora duara kubwa ardhini kwa mchanganyiko wa majivu, damu ya kuku na majani ya mitishamba ya pekee. Katikati ya duara hilo aliweka hirizi mbili kubwa na tufe la kioo lililoonekana kung'aa hata gizani

"Katika ibada hii tutakabili roho za kisasi..mmoja wenu lazima awe tayari kutoa dhabihu kubwa ili kuvunja mkataba wa laana hii"

Maneno hayo yalizua hofu miongoni mwa waliohudhuria, Karungi alimtazama Baruti kwa wasiwasi

"Hii inamaanisha nini" aliuliza kwa sauti ya chini

"Inamaanisha kuwa mmoja wetu anaweza kupoteza uhai wake ili kuokoa familia yetu" Baruti alijibu kwa sauti thabiti, macho yake yakiwa yameshikwa na uthabiti wa ajabu

***************************

Wakati mzee Mbalamwezi alipowasha mishumaa mitano iliyoizunguka duara, upepo wa ghafla ulianza kuvuma kwa nguvu. Moshi mweusi ulijaa angani na sauti za kutisha zilianza kusikika. Roho za kisasi zilijitokeza zikifuatana na mngurumo wa radi na kicheko cha kejeli

"Karungi...hatujawahi kusamehe usaliti wako" sauti ya roho moja ilisikika ikitoka kwenye kivuli kirefu kilichokuwa kimejitokeza karibu na duara

"Nipo hapa kwa msamaha" Karungi alijibu kwa sauti iliyojawa na hofu.... "Nipo hapa kuomba huruma yenu"

Baruti alisimama imara katikati ya duara..

"Laana hii haitabaki milele niko tayari kukabiliana nanyi ili kulinda kizazi changu"

Roho zile zilicheka kwa dhihaka..

"Na unadhani unaweza kushinda"

Baruti aliposhika hirizi yake kwa nguvu, mwanga wa dhahabu ulitoka ndani yake ukiangaza duara lote. Roho zile zilianza kushambulia zikirusha upepo na sauti za kutisha lakini kila mara Baruti alikumbuka maneno ya baba ake..

"Mwokozi wa familia ni yule mwenye dhamira safi"

Alipiga magoti akaomba kwa moyo wote huku mwanga wa hirizi ukizidi kuwa mkali. Roho zile zilianza kushuka nguvu zikilia kwa maumivu makali

Mwisho, zilipotea kabisaaaa zikifuatana na sauti ya kishindo kikubwa

Mbalamwezi alitazama kila kitu kwa mshangao..

"Umefanikiwa Baruti. Ulikuwa na dhamira safi ya kupambana kwa ajili ya familia yako...roho zimekubali kushusha laana"

Karungi alianguka sakafuni kwa machozi ya furaha..

"Asante Baruti umeokoa maisha etu"

Lakini Baruti alitabasamu kwa uchovu..

"Hii ilikuwa kwa ajili ya familia etu, hatutakiwi tena kuishi katika kivuli cha laana"

Baruti alikubali dhamira yake lakini bila kujua, giza la zamani lilikuwa bado halijakufa kabisa...

*JE NINI KINAENDELEA*...

*USIKOSE SEHEMU YA 5*
[12/12, 10:16 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA: 2024/2025*
*SMS & WHATSAPP: 0752474397*

*SEHEMU YA TANO*

*ILIPOISHIA*

Baruti alikubali dhamira yake lakini bila kujua, giza la zamani lilikuwa bado halijakufa kabisa..

Baada ya ibada hiyo Baruti alijiona mkombozi wa familia yake akiamini kuwa mapambano ya kiroho waliyoshinda yameweka kikomo kwa laana iliyokuwa inatesa familia yao kwa vizazi lakini licha ya hisia za ushindi alijua kuwa giza la zamani halikuwahi kuwa mbali

Muda ulizidi kupita, mambo ya ajabu yalianza kujitokeza. Kwa siku kadhaa nyumba ya familia ilianza kujazwa na kivuli kizito cha wasiwasi. Kila walipokaa pamoja hali ilionekana kuwa nyepesi lakini waligundua kuwa hisia ya hatari ilikuwapo. Mambo yaliyoonekana kuwa ya kawaida kama vile upepo mwepesi na sauti za ndege usiku yaligeuka kuwa ya kutisha. Karungi aliweza kuhisia mabadiliko hayo akijua kuwa hakuna kilichomalizika

Mara moja sauti ya ngurumo ya radi ilitikisa angani huku kivuli cha mtu mrefu kilichotokea kutoka nje ya nyumba kilileta mshtuko kwa familia. Hii ilikuwa ni ishara ya kutosha kuwa roho za kisasi bado hazikuwa zimeachilia mbali familia hiyo. Karungi alijua kuwa lazima wajitokeze tena ili kuumaliza kabisa

“Baruti..kuna kitu kimejaa angani sijui kama tutapata amani, giza hili halijakamilika” alisema Karungi kwa sauti ya hofu akimuangalia Baruti kwa macho yaliyojaa wasiwasi

Baruti alijua kuwa safari yao ilikuwa bado haijaisha, alienda kwa mzee Mbalamwezi kwa haraka akimwambia kwamba familia yao ilikuwa bado inakumbwa na vita vya kiroho. Mzee aliguswa akasema..

"Giza lilio nyuma yako halijaisha bado lazima tuendelee kufanya kazi kubwa"

Wakiwa wamejizatiti kwa maombi na michakato ya kiroho, Baruti alijua kuwa hatua yao ya mwisho ilikuwa ikikaribia. Hakuwa tayari kuona familia yake ikiguswa tena na roho za kisasi lakini alijua kuwa kumaliza vita hii kutahitaji dhabihu ya kipekee

Katika usiku uliojaa upepo wa kushtua Mbalamwezi alikusanya tena familia aliwaambia kuwa ili kumaliza kabisa roho za kisasi walihitaji kufanya dhabihu ya mwisho. Walipaswa kuchukua hatua kubwa ili kupinga kile kilichokuwa kinatokea

“Ndugu zangu, bila dhabihu ya mwisho, roho hizi hazitakufa” alisema mzee kwa sauti ya nguvu

“Kwa jina la familia tunapaswa kutoa kitu cha kipekee ili roho hizi zielewe kuwa hatuko tena kwenye kifungo chao”

Baruti alijua kuwa wakati wa kufunga vita ilikuwa umefika, alipewa jukumu la kuchukua hatima ya familia yake lakini alijua kuwa hii ilikuwa ni hatua ambayo ingeweza kumgharimu maisha yake

“Kwa ajili ya familia yetu nitatoa kile kilicho cha muhimu” alisema kwa uthabiti

Kwa moyo wa dhamira safi, Baruti alikusudia kumaliza vita hii kwa ushindi wa mwisho lakini je, dhabihu aliyokuwa anajiandaa kutoa itakuwa ya kutosha kumaliza kabisa mapambano haya??

JE NINI KINAENDELEA...

USIKOSE SEHEMU YA 6
[12/12, 10:17 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA: 2024/2025*
*SMS & WHATSAPP: 0752474397*

*SEHEMU YA SITA*

*ILIPOISHIA*

Baruti alijua kuwa wakati wa kufunga vita ulikuwa umefika alipewa jukumu la kuchukua hatma ya familia ake lakini alijua kuwa hii ilikuwa ni hatua ambayo ingeweza kumgharimu maisha yake

Katika giza la usiku, familia ya Baruti ilikusanyika tena kwenye duara lililochorwa kwa majivu na damu ya kuku. Mbalamwezi aliongoza ibada hiyo akiwa na uso wa uzito. Maji ya upole yalipokuwa yanakatisha giza roho za kisasi zilikuwa zikijitokeza tena zikicheka kwa dhihaka

"Unadhani hii itakufikisha wapi Baruti? Roho zetu zitaendelea kutawala" sauti za roho zilizungumza kwa kasi zikileta hisia za uoga miongoni mwa familia

"Hatutakiwi tena kuishi katika kivuli cha laana" Baruti alikalia kwa nguvu macho yake yakiangaza kwa mwangaza wa hirizi aliyoshikilia

Mbalamwezi alionekana kuwa na wasiwasi akijua kuwa ili kuvunja kabisa giza hili lazima dhabihu ya kipekee itolewe

"Baruti wakati umefika lakini dhabihu yako itakuwa ya kipekee na yenye maumivu. Kitu cha kipekee kitahitajika kuimaliza roho hii ya kisasi" alizungumza kwa sauti nzito huku akiwangalia kwa jicho la uangalifu

Karungi alikusudia kusema kitu lakini aligundua kuwa hakuna neno la kusema mbele ya dhabihu iliyokuwa inajiandaa. Alijua kuwa Baruti alikuwa na dhamira safi lakini haikuwa rahisi kubeba mzigo wa kumaliza mapambano haya

Kwa hatua kubwa na imani isiyoyumba Baruti alijua kuwa lazima aonyeshe upendo wa dhati kwa familia yake lakini kwa gharama ya yeye mwenyewe aliamua kuwa dhabihu ya mwisho ingeweza kumaliza giza hili la kisasi ambalo lilikuwa likiwatesa kwa vizazi vingi, alienda katikati ya duara la majivu na damu akiongozwa na maneno ya baba yake

"Mwokozi wa familia ni yule mwenye dhamira safi"

Alifanya maombi kwa nguvu akijua kuwa roho za kisasi zilikuwa zinajiandaa kushambulia kwa nguvu zote. Katika hatua hii Baruti alijua kuwa hata kama angekufa familia yake ingekuwa salama

Mbalamwezi alikusanya nguvu zake zote na kuongoza ibada kwa mafundisho ya nguvu za kiroho. Upepo mkali ulianza kuvuma na roho za kisasi zilijitokeza kwa kishindo kikubwa. Kila roho ilikuwa ikijaribu kumshambulia Baruti lakini alikataa kurudi nyuma

Muda ulivyozidi kupita mwanga wa hirizi ulizidi kung'aa kwa nguvu. Baruti alikusudia kutekeleza dhabihu huku akijua kuwa familia yake ilikuwa na matumaini makubwa kwake hata hivyo roho za kisasi zilijitokeza kwa nguvu ya ajabu zikiwacheka kwa dhihaka

"Utavua wapi nguvu zako za kupigana" sauti za roho zililalamika lakini Baruti alijua kuwa hakuna kingine kilichobaki zaidi ya kutoa dhabihu hiyo

Akiwa na maombi ya kipekee alifanya tendo la kumaliza mapambano. Roho za kisasi zilishtuka zikilia kwa maumivu makali na kuanza kutoweka mwishowe, giza la zamani lilijitokeza kwa kishindo na Baruti alijua kuwa familia yake ilikuwa imeokolewa

"Hatimaye giza limeondoka na laana imevunjika" alisema Mbalamwezi kwa sauti ya furaha akimtazama Baruti kwa shukrani lakini Baruti alikuwa kimya akiangalia familia yake kwa macho ya huzuni na furaha, aliamini kuwa kumaliza laana ilikuwa ni ushindi mkubwa lakini alijua kuwa kumaliza mapambano ya kiroho haya hakukuwepo tena nyuma ya familia yake

Walikuwa wameshinda lakini kwa gharama ya juu...

*USIKOSE SEHEMU YA 7*
[12/12, 10:18 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA: 2024/2025*
*SMS & WHATSAPP: 0752474397*

*SEHEMU YA SABA* 

*ILIPOISHIA*

Hatimae giza liliondoka na laana ya familia ya Kirama ilivunjwa, mwanga wa hirizi ulipotea polepole na upepo mkali ulitulizana. Wakati familia ikijaribu kusherehekea ushindi, kilio cha Baruti kilianza kusikika katikati ya duara la majivu

Mbalamwezi alimkimbilia kwa haraka

“Baruti...umefanya mengi kwa familia hii umevunja mnyororo wa laana lakini... unajisikiaje sasa”

Baruti alitabasamu kwa uchovu huku macho yake yakijaa maji

“Sina maumivu ya mwili lakini nafsi yangu imechoka. Najua laana haipo tena lakini kuna kitu bado... bado nakiona giza ndani yangu”

Karungi alimsogelea huku akiwa na machozi..

“Baruti umetupigania. Bila wewe hatungeweza kuishi maisha haya mapya lakini tafadhali unamaanisha nini unaposema kuna giza”

Baruti alinyamaza kwa muda akitazama ardhi iliyochafuka na majivu kisha kwa sauti ya chini sana alisema..

“Mbalamwezi hakuniambia kila kitu. Kuna gharama ya kuvunja laana si ya damu bali ya roho yangu, sijui kama nitakuwa salama baada ya hii”

Mbalamwezi alishtuka uso wake ukionyesha wasiwasi

 “Baruti hii haipaswi kuwa hivi..dhamira safi ya moyo wako ndio iliyovunja laana si lazima ulipe kwa roho yako”

Lakini kabla ya kuendelea, sauti ya mwanamke ilisikika kutoka gizani ilikuwa sauti ya uchungu na ghadhabu

“Baruti umevunja mkataba lakini haujafanikisha kila kitu”

Wote waligeuka na kivuli cha mwanamke mzee kiliibuka katikati ya mti mkubwa uliokuwa karibu na uwanja..

"Mimi ni Nyarara, mlinzi wa mkataba wa laana ya Kirama. Mkataba umevunjwa lakini kuna masalia. Damu ya Baruti haiwezi kutosha. Mtoto wa Kirama atakuwa kifungo kipya cha familia”

Karungi alisimama kwa hasira

“Hapana tumevumilia vya kutosha Baruti hafai kulipa chochote tena na mtoto wake hatahusika kwenye laana yoyote”

Baruti aliinuka kwa nguvu zilizobaki

"Nyarara, kama kuna jambo la mwisho nilipaswa kujifunza.. ni kwamba familia yangu ni mali yangu. Sitakubali tena roho au giza kukandamiza ukoo wetu”

Kabla ya kusema zaidi, Nyarara alirusha moshi mzito kuelekea kwao na kila mmoja alihisi uzito wa maamuzi yao ya awali. Baruti kwa mara nyingine alichukua hirizi iliyokuwa tayari imezimika na kuinua juu. Mwanga dhaifu ulianza kutoka lakini nguvu za Baruti zilionekana kupungua polepole

*JE, BARUTI ATAWEZA KUKABILIANA NA NGUVU MPYA ZA NYARARA?*

*USIKOSE SEHEMU YA NANE*
[12/12, 10:19 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA 2024/2025*
*SMS & WHATSAPP: 0752474397*

*SEHEMU YA NANE*

*ILIPOISHIA SEHEMU YA 7*

Kabla ya kusema zaidi, Nyarara alirusha moshi mzito kuelekea kwao na kila mmoja alihisi uzito wa maamuzi yao ya awali. Baruti kwa mara nyingine alichukua hirizi iliyokuwa tayari imezimika na kuinua juu. Mwanga dhaifu ulianza kutoka lakini nguvu za Baruti zilionekana kupungua polepole

*ENDELEA...*

Baruti alitetemeka huku mwili wake ukionekana kushindwa na mzigo wa nguvu za Nyarara. Giza lilikuwa zito likifunika kila kona ya uwanja huo. Pumzi zake zilikuwa nzito lakini ndani yake kulikuwa na moto wa matumaini ambao haukuwa tayari kuzimwa

"Nyarara" Baruti aliongea kwa sauti dhaifu lakini thabiti.. "Sitaogopa. Damu yangu ni zaidi ya mikataba ya giza uliyoifanya familia yangu itaishi huru"

Nyarara alicheka kwa kejeli, sauti yake ikizidisha hofu katika mioyo ya waliokuwa wakishuhudia

"Unadhani una nguvu ya kunizuia? Roho ya ukoo wako imenitumikia kwa karne nyingi. Wewe ni nani kunipinga"

Karungi akiwa amesimama pembeni, aliona macho ya Baruti yakianza kuzimika

Kwa hofu kuu alipaza sauti

"Baruti kumbuka maneno ya baba yako, kumbuka kuwa hofu ni mfungwa wa roho. Usiruhusu hofu ishinde"

Baruti alikumbuka haraka maneno ya baba yake marehemu aliyemtia moyo siku zote kujikomboa na kuchagua mwanga badala ya giza. Alijilazimisha kusimama akashika hirizi yake kwa nguvu zaidi na kusema kwa sauti ya imani

"Nguvu zako haziwezi kuzidi upendo wa damu yangu kwa familia yangu"

Mwanga wa hirizi ulianza kung'aa zaidi ukisambaa na kuvunja moshi wa giza uliokuwa ukimzunguka. Kila hatua ya Baruti ilizidi kuifanya nuru hiyo kuwa imara zaidi. Nyarara alianza kurudi nyuma akijaribu kupinga nguvu inayomzidi

Lakini kabla ya mwanga huo kumaliza kazi yake Nyarara alirusha mngurumo wa ghafla na upepo mkali ulivuma kwa kasi ukimsukuma Baruti chini. Hirizi ilidondoka kutoka mikononi mwake na mwanga wake ukaanza kuzimika tena

"Huwezi kushinda vita hii" Nyarara alirudia kwa ghadhabu

"Hii ni laana ya kizazi chenu na haiwezi kuondolewa kwa urahisi"

Karungi alimkimbilia Baruti akamshika begani huku machozi yakimtiririka

"Simama Baruti familia yetu inakutegemea. Hirizi ni chombo tu lakini nguvu ya kweli iko ndani yako"

Maneno hayo yalimgusa Baruti kwa undani akifunga macho na kutamka kwa sauti thabiti

"Sihitaji hirizi ili kushinda. Imani yangu na upendo wangu kwa familia yangu ni silaha yangu kuu"

Mara Baruti aliposema maneno hayo mwanga wa dhahabu ulitoka kutoka moyoni mwake ukisambaa haraka zaidi kuliko mwanga wa hirizi. Nyarara alipiga kelele za maumivu, kivuli chake kikiyeyuka hatua kwa hatua

"Imani yako imenishinda..." Nyarara alisema kwa sauti dhaifu kabla ya kupotea kabisa. Uwanja ulirudi kuwa kimya na hewa ya utulivu ilichukua nafasi ya moshi mzito wa giza

Karungi alimkumbatia Baruti akilia kwa furaha

"Umefanikiwa Baruti, umevunja laana ya ukoo wetu"

Mbalamwezi aliyekuwa akishuhudia kwa mbali alikubali kwa kichwa huku akisema

"Baruti umeonyesha ujasiri wa kweli. Ukoo wa Kirama hautaishi tena chini ya kivuli cha giza"

**************************

Asubuhi ilichomoza na kwa mara ya kwanza familia ya Kirama ilihisi uhuru wa kweli. Baruti alisimama kwa shida lakini akiwa na tabasamu akitazama jua likipambazuka

"Tumefanikiwa" alisema kwa sauti ya unyenyekevu...

Lakini Karungi akiwa na macho ya shaka alimuuliza

"Je, laana imeisha kabisa au kuna jambo lingine linaweza kutokea"

Baruti alitabasamu kwa uchovu

"Hili ni jambo tunalopaswa kulijua tu kwa wakati"

*MWISHO WA SEHEMU YA NANE*

*JE, KUNA HATARI MPYA INAYOKUJA? NA FAMILIA YA KIRAMA ITAKABILIANA VIPI NA MAISHA BILA LAANA?*

*USIKOSE SEHEMU YA TISA*
[12/12, 10:19 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA 2024/2025*
*SMS & WHATSAPP: 0752474397*

*SEHEMU YA TISA*

*ILIPOISHIA SEHEMU YA 8*

"Je laana imeisha kabisa au kuna jambo lingine linaweza kutokea"

Baruti alitabasamu kwa uchovu..

"Hili ni jambo tunalopaswa kulijua tu kwa wakati"

*ENDELEA*

Wiki mbili baada ya ushindi wao kijiji cha Mwikambe kilionekana kutulia. Shughuli za kawaida zilirejea watu walilima mashamba, watoto walicheza huku wakiimba nyimbo za kijiji na wazee walikusanyika chini ya mti wa mkorosho kwa mazungumzo hata familia ya Kirama ilianza kufurahia utulivu

Lakini nyuma ya tabasamu za kijijini kulikuwa na dalili zisizoeleweka. Kila usiku upepo wa ajabu ulikuwa ukipeperusha milango na madirisha ya nyumba za kijiji. Kulikuwa na milio ya ajabu usiku wa manane kama sauti za nyoka wakisonga kwenye ardhi

Siku moja Nyarobe rafiki wa karibu wa Baruti alimtembelea akiwa na uso wa wasiwasi..

"Baruti, jana usiku tulisikia sauti za kilio kutoka msituni karibu na mto tulidhani ni wanyama lakini tulipojaribu kuangalia tuliona kivuli kikubwa kikizunguka inawezekana nini kinaendelea"

Baruti alikosa maneno ya kujibu alikumbuka kilichotokea wiki mbili zilizopita na akahisi kwamba kuna kitu hakikuwa sahihi

Baruti na Karungi walikaa usiku wa manane kujadiliana. Karungi alikuwa kimya, uso wake ukiwa umejawa na hatia mwishowe alimwambia Baruti

"Nadhani kuna jambo ambalo unapaswa kujua. Kabla baba yetu hajafa nilifanya makubaliano..."

Baruti alimsikiliza kwa mshangao na huzuni..

"Makubaliano gani Karungi mbona hukusema"

Karungi alisimulia kwa undani jinsi alivyofanya mkataba na mganga wa giza ili kuokoa familia yao baada ya kifo cha baba

"Niliahidi kwamba nitatoa sadaka yoyote ili familia yetu isiharibike nilidhani nilifanya jambo sahihi kwa wakati huo lakini sijui matokeo yake"

Baruti alihisi huzuni na hasira kwa wakati mmoja

"Karungi umetuangamiza sasa tunapaswa kufanya nini"

Alienda moja kwa moja kwa Mbalamwezi akimuomba msaada. Mbalamwezi aliwaambia kuwa nguvu za giza zilipata mwanya kupitia mkataba wa Karungi

"Mkataba huu hauwezi kuvunjwa bila kujitoa dhabihu kubwa" alisema kwa sauti nzito

"Ni dhabihu gani" Baruti aliuliza, tayari kwa lolote

Mbalamwezi alimuelekeza kwamba walipaswa kurudi kwenye mti wa laana ulioko msituni na kuomba radhi kwa roho za ukoo wao

Hata hivyo safari hiyo ilikuwa hatari kwani roho za giza zilikuwa zikivizia

Baruti na Karungi walikusanya ujasiri na kuanza safari yao kuelekea kwenye mti wa laana. Njiani walihisi kuwa walikuwa wakifuatwa

Kila wakati waliposimama, sauti za majani yakisogezwa zilikuwa zikisikia lakini hawakuweza kuona chochote.
Walipofika kwenye mti kila kitu kilikuwa kimya. Baruti alisimama karibu na mti akiweka hirizi mikononi mwake

"Roho za ukoo wangu nakuja kwa unyenyekevu. Naomba uiachilie familia yangu kutoka kwa minyororo ya giza"

Ghafla upepo mkali ulivuma na sauti ya Nyarara ilisikika

"Baruti unadhani unaweza kuondoka hivi tu..kuna deni kubwa lililoahidiwa lazima liwepo"

Baruti aliweka mikono yake juu ya hirizi na kuiweka karibu na kifua chake. Mwanga mkali ulitoka na Nyarara alianza kudhoofika

"Nimechoka kuwa mtumwa wa laana hii!" Baruti alilia kwa uchungu

Nyarara alijitokeza kwa nguvu kubwa akiwa na sura ya kutisha zaidi kuliko awali alielekea moja kwa moja kwa Karungi akisema

"Wewe ndie uliahidi damu sasa deni lako limenifikia"

Baruti alimzuia kwa kupiga kelele

 "Achana nae Nyarara deni ni langu sasa. Chukua damu yangu badala yake"
Nyarara alicheka kwa sauti ya dharau

"Wewe ni mjasiri Baruti lakini swali ni hili..Je, uko tayari kufa kwa ajili ya familia yako"

Baruti aliweka mikono yake juu ya hirizi na kuiweka karibu na kifua chake. Mwanga mkali ulitoka na Nyarara alianza kudhoofika

"Nimechoka kuwa mtumwa wa laana hii Baruti alilia kwa uchungu

Baruti alihisi nguvu zikiendelea kuongezeka ndani yake akielewa kuwa ni lazima amshinde Nyarara kabisa. Hirizi ilining'inia na kila mwanga ulipomuingia Baruti, roho za ukoo zilionekana kuwa pamoja nae. Sauti za kale zilisikika zikimwambia kuwa yeye ndie ufunguo wa uhuru

Nyarara alihisi mwanga huo akajitahidi kumzuia Baruti kwa kila njia

"Hapana, hapana usinitendee hivi" alijitahidi kusema huku akianguka chini. Damu ilimtoka kutoka mdomoni na Nyarara alinyamaza kwa miongo mirefu.
Baruti alifungua macho kwa hofu, akijua kuwa ushindi ulikuwa wake

"Laana imekwisha" alisema kwa sauti ya nguvu "Damu yangu itakuwa dhamana ya kuwakomboa wenzangu kutoka minyororo ya roho hizi"

**************************

Familia ya Kirama ilihisi mabadiliko ya ghafla. Watu wa kijiji walikusanyika karibu na mti wa laana wakiangalia jinsi Baruti alivyopambana na nguvu za giza. Mwanga uliotoka kwa Baruti ulipotea lakini Nyarara hakurudi tena

Roho za ukoo walitowekana kijiji kilijaa sauti za furaha. Karungi alilia kwa furaha akihisi kuwa amekwisha kuokoa familia yao kutokana na hukumu ya zamani. Baruti aliposhuka uso wake ukawa na tabasamu la huruma

"Sasa hakuna tena laana"

Baruti alisema kwa upole. "Tumepata amani kamili"

MWISHO WA SEHEMU YA TISA

Je, Baruti atamudu kumaliza mkataba huo bila kupoteza maisha yake na nini hatma ya familia ya Kirama?

*USIKOSE SEHEMU YA KUMI (FINAL)*
[12/12, 10:20 PM] Justin Baruti: *UTUNZI WA RIWAYA: DAMU YA KIFAMILIA*
*MTUNZI: JUSTIN BARUTI*
*MWAKA: 2024/2025*
*SMS & WHATSAPP: 0752474397*

*SEHEMU YA 10 (FINAL)*

*ILIPOISHIA*

Roho za ukoo walitoweka na kijiji kilijaa sauti za furaha. Karungi alilia kwa furaha akihisi kuwa amekwisha kuokoa familia yao kutokana na hukumu ya zamani. Baruti aliposhuka uso wake ukawa na tabasamu la huruma

"Sasa hakuna tena laana Baruti alisema kwa upole...tumepata amani kamili"

Mchana ulipokuwa ukianza kupenya Baruti aliweka mikono ake juu akitamka maneno ya shukrani kwa Mungu na roho za ukoo

"Mungu nashukuru kwa nguvu ulizotujalia. Tumepona kutoka kwa laana hii"

Watu wa kijiji walikusanyika wakimuangalia kwa heshima wakijua kuwa ni yeye aliyeleta mwisho wa kipindi hiki kigumu. Karungi alimtazama Baruti kwa upendo na shukrani

"Shukrani Baruti umenifanya niwe na amani moyoni mwangu...familia yetu sasa ni huru"

Hata hivyo Baruti alihisi kuwa hakupona kikamilifu alijua kuwa upendo wa kweli na mshikamano wa watu wa kijiji ndio nguvu inayoweza kudumu. Alisimama mbele ya kijiji na kusema

"Laana imeondoka lakini tunahitaji kuishi kwa umoja na huruma kwa kila mmoja wetu. Hii ndio nguvu tunayohitaji sasa"

Kijiji kilimshangilia Baruti na kila mmoja aliangalia maisha mapya akiwa na matumaini. Nyarobe alijua kwamba maisha yao yatabadilika milele lakini sasa walikuwa na uhakika wa nguvu zinazotoka kwa mshikamano

Baada ya siku hiyo ndefu Baruti alikaa kimya akiwa na Karungi pembeni yake wakitafakari matukio yote yaliyopita

"Karungi nimekuelewa sasa. Dhamira yako ilikuwa safi lakini njia ilikuwa na dhahabu nyingi. Ni mshikamano tu ndio utatupeleka mbele"

Karungi alilia kwa furaha

"Baruti umeniongoza kwa mwangaza...sijui ni wapi tunapokwenda lakini pamoja tutapambana na changamoto yoyote"

Baruti alishika mikono ya Karungi kwa upole

"Tutaanza upya Karungi na kila mmoja wetu atakuwa nguvu ya mwenzake"

**************************

Siku ya mwisho ilifika kwa kijiji cha Mwikambe. Uwanja wa kijiji uliokuwa umeketi kwa watu ulijaa sauti za furaha na vicheko lakini ndani ya mioyo ya watu kuna wasiwasi wa kijusi ambao haukutoweka. Ilikuwa ni sauti ya wanyama wa mwituni ambao walionekana kuja karibu zaidi na kijiji cha Mwikambe

Nyarara, mke wa kale wa Kirama alikuwa bado yupo. Siku ya mwisho alitokea akiwa na nguvu kubwa zaidi kuliko hapo awali alionekana mng’ao wa giza na mvumo wa upepo ulipita angani

"Nimekuja tena Baruti" alisema kwa sauti ya kutisha

"Laana haitoweki kwa urahisi nawaombeni damu, damu zaidi"

Baruti alisimama akitabasamu akijua kuwa ni wakati wa kupambana

"Nyarara huwezi tena kutuvuruga damu yetu imekuwa yenye nguvu zaidi sasa"

Sauti za kijiji zilikuja pamoja wakimjibu Baruti kwa mshikamano. Wanasimama wote kwa mshikamano wa familia wakisema kwa sauti moja

"Hatutakubaliana na laana hii tena"

Baruti akachukua hirizi yake na kutamka kwa nguvu

"Nyarara endelea mbele lakini laana yako itamalizika sasa"

Kwa mwanga mkali uliotoka Nyarara alisikia kelele za muktadha wa kijiji na ghafla aliumia kwa maumivu makali alitikiswa na nguvu zake mwenyewe na mwishowe akapotea ndani ya giza

Watu wa kijiji walipiga makofi kwa furaha wakijua kuwa wamesimama kwa mshikamano. Baruti alibeba kijiti chake na kusema

"Laana imeondoka kabisa lakini mshikamano wetu utaendelea kuwapa nguvu daima"

**************************

Siku zilipita lakini kijiji cha Mwikambe kilibaki kuwa na macho ya makini. Wanyama wa mwituni waliendelea kuzunguka kijiji lakini watu walijifunza kuishi kwa mshikamano wakifahamu kuwa nguvu yao ni umoja na upendo

Baruti na Karungi walitambua kuwa vita vya giza havitakoma lakini pamoja wangeweza kudumu milele. Na kwa mshikamano wao wakajua kuwa kijiji chao kingekuwa salama milele

*MWISHO*

Post a Comment

Previous Post Next Post