Baada ya will Kuona afya ya mkewe inazidi kuzorota,jitihada zote za kutafuta pesa kwaajili ya operation ya mkewe zimegonga mwamba ikabidi afike moja kwa moja kwa nduguye Dan kuomba asaidiwe pesa za matibabu ya mkewe
Alikaribishwa vizuri nyumbani kwa Dan Kisha akamueleza shida iliyo mpeleka, hakujua utajiri alionao Dan kaupata wapi,kumbe siku hiyo Dan na cruel yake walikuwa na mchongo wa kwenda kupiga tukio kwenye benk moja iliyokiwa inataka kuhamisha pesa kwenda benk nyingine
Hivyo Dan akamtaka will wajumuike wote kwenye mission hiyo ili apate zaidi ya pesa anayohitaji kwaajili ya matibabu ya mkewe,Will alikuwa mbishi,ila kwa sababu ya situation mbaya aliyokuwa nayo ikabidi akubali kuambatana na Cruel ya Dan
Wakafika moja kwa moja mpaka benk,zoezi la uvamizi halikuwa gumu sababu walikuwa professional,wakafanikiwa kuweka benk hiyo chini ya ulinzi na kupora kiasi Cha pesa Cha kutosha
Kumbe Kuna askari huwa anammezea mate muhudumu wa benk hiyo na hiyo siku alikuwa anaenda kujaribu bahati yake ,bila kujua benk hiyo ipo chini ya ulinzi, alipojaribu kuingia benk alizuiwa na Dan akijidai ni mfanyakazi wa benk hiyo na kwamba siku hiyo hamna huduma
Ila askari huyo akalazimisha akidai ana shida ya dharula,wakamruhusu aingie,baada ya askari huyo Kuona hali ya tofauti benk hapo tayali alikuwa kachelewa na akadhibitiwa kabla hajamsanua askari mwenzake anayemsubir nje ya bank
Baada wa rafiki wa askari huyo Kuona mwenzake aliyeingia bank hapo yupo mikononi mwa watu ambao haelewi sura zao moja kwa moja akajua bank ipo chini ya wakulungwa, hivyo akatoa taarifa haraka kwa maaskari wengine
Ndani ya muda mfupi bank ikazungukwa na maaskari ndani na nje,ndani ya muda mfupi waharifu waliojaribu kujibu mashambulizi wakawa chini,akabaki Dan na will wakiwa na yule askari mateka wakimtumia kama ngao
Dan alipojisahau kidogo askari huyo akamuwai akijaribu kujiokoa,Bahati mbaya akapigwa risasi wakamuacha akiugulia na kuendelea na jitihada nyingine za kujaribu kuchomoka Salama benk hapo,bahati nzuri walishuhudia ambulance moja ikitoka benk humo wakaona ndio njia rahisi ya wao kutoka bila kusanukiwa
Ikabidi waiteke ambulance hiyo iliyokuwa na mtoa huduma na mgonjwa ambae ndio yule askari mwenye bahati mbaya waliyemjeruhi ,kisha will akashikilia usukani wa ambulance hiyo na kufanikiwa kutoka salama
Utamu wa movie hii ni baada ya Ambulance iliyowapakia will na Dan kusanukiwa baada ya aliyekuwa dereva wa ambulance hiyo kukutwa kapigwa vibaya na kina Dan na kuporwa ambulance hiyo
Hii movie nzima ni mchakamchaka na mtafuno baina ya vikosi vya usalama kuungana ili kuwanasa waharifu hao,katika movie za waporaji bank nilizowai Kuona hii ni mashine
Tags:
movies