Hadithi inaanza siku ya maadhimisho ya ndoa ya Nick na Amy Dunne. Amy anatoweka ghafla, na hali hiyo inachochea msako mkubwa na uchunguzi wa polisi.
Huku vyombo vya habari vikiangazia tukio hilo, ushahidi unaanza kumwelekeza Nick kuwa mshukiwa mkuu wa kifo au kutoweka kwa mke wake. Hata hivyo, kadri uchunguzi unavyoendelea, hadithi ya Amy na Nick inaonyesha giza la ndani ya ndoa yao — uongo, usaliti, na hila za kisaikolojia.
Plot twist kubwa inakuja pale ambapo inabainika kwamba Amy hakuwa ametekwa wala kuuawa; alijiteka mwenyewe kwa hila kali ili kumkomoa Nick kwa sababu ya usaliti wake. Amy anajua jinsi ya kucheza na akili za watu na vyombo vya habari ili kuonyesha Nick kama mhalifu. Mwisho wa filamu ni wa kushangaza na wa kufikirisha kwani Amy anarejea nyumbani kwa Nick na kumlazimisha kuendelea kuwa naye kwa hofu na vitisho.
Tags:
Movie