• Home
  • About Us
  • Contact Us
JOEBOY STUDIO
  • Home
  • Download App
Slide 1 Slide 2 Slide 3 Slide 4 Slide 5 Slide 6 Slide 7 Slide 8 Slide 9 Slide 10
Small Slide 1 Small Slide 2 small slide 3 Small Slide 4 Small Slide 5
Big Image
Series kali za kizungu, kikolea, kinaijeria zinapatikana kama zote
Small Top
Graphics
Small Bottom
Movie's
Ulimwengu wa Simulizi

Hii ni kwawadau wanaopenda kusoma simulizi bonyeza button hiyo juu kisha chagua aina ya simulizi..

Big Image
Series kali za kizungu, kikolea, kinaijeria zinapatikana kama zote
Small Top
Graphics
Small Bottom
Movie's
HomeRiwaya

FUMBO LA NDOA

byJOEBOY -January 01, 2025
0
UTUNZI WA RIWAYA: FUMBO LA NDOA
MTUNZI: JUSTIN BARUTI
MWAKA: 2024/2025
WHATSAPP: 0752474397

UTANGULIZI

Kila mwanamke anaingia kwenye ndoa akiwa na ndoto za furaha, amani na upendo. Katika baadhi ya jamii ndoa sio tu hatua ya kimaisha bali ni matarajio makubwa yanayotegemewa na familia, jamii na kila mwanamke mwenyewe. Lakini je, ni kwanini baadhi ya wanawake uishi maisha ya majuto huku wengine wakiwa na furaha?

Katika simulizi hii ya Justin Baruti tutaingia ndani ya safari ya ndoa kupitia macho ya Mariam, mwanamke aliyekutana na changamoto ambazo wanawake wengi hawajui kabla ya kusema *ndio*

Fuata simulizi hili ili kuelewa fumbo hili lenye siri kubwa

*SEHEMU YA 1*

Alikuwepo binti mmoja kijijini Mugumu jina lake Mariam alikuwa na umri wa miaka 25, binti mrembo mwenye ndoto kubwa za maisha bora ndani ya ndoa. Kijiji hiki kilijulikana kwa jamii yake inayopenda sherehe za harusi na matarajio makubwa kutoka kwa wanawake wa kijiji icho. Mariam alitamani sana siku moja kuolewa, kuanza safari ya maisha ya pamoja na mpenzi aliyekuwa na heshima na upendo

Lakini safari ya ndoa sio rahisi kama ilivyotazamwa na wengi au wengi wanavyodhani. Mariam alijua hilo vema akijitayarisha kwa mawazo mbalimbali akijiuliza mara kwa mara ni kwa nini wanawake wengi uishi maisha ya majuto baada ya ndoa? Je, ndoto zake za maisha bora ndani ya ndoa zingeweza kufanikishwa?

Mariam alikua na ndoto za mpenzi ambae angesimama nae wakijenga maisha ya pamoja kwa furaha na upendo. Ndoto za ndoa kwake zilikuwa za amani, familia yenye furaha na watoto waliobarikiwa lakini mara nyingi mambo hayaendi kama alivyoyategemea

Siku moja wakati kijiji kizima kikiandaa sherehe za harusi kwa shauku, Baruti mwanaume maarufu kwa heshima yake kijijini alifika nyumbani kwao Mariam akiwa na zawadi za kawaida ikiwemo unga wa mahindi na sukari lakini hata hivyo kusudi lake halikuwa hili bali alitokea kumpenda Mariam kwa moyo wake wote, taratibu alianza kumtongoza

“Mariam umekua sasa nahisi wakati umefika” alisema Baruti kwa sauti nyororo

Mariam alimuangalia kwa tahadhari kwa upendo alikuwa nao lakini bado hakuwa na uhakika kama Baruti ndie mtu sahihi wa maisha yake aliyekuwa akimtafutia maisha bora

Alikumbuka maneno ya mama yake aliyekuwa amekwisha dhihirisha matarajio ya kijiji kwamba ndoa lazima ifanyike.. akamtafuta mama yake

“Mama kwanini unaamini kwamba Baruti ndie chaguo bora” aliuliza kwa sauti ya chini akiwa na hofu

“Mariam sio tu kuhusu Baruti, ni kuhusu heshima yako kama mwanamke. Maisha ya kijiji hiki yanakutegemea uolewe mapema na mtu mwema” mama yake alijibu akiwa na hakika

**************************

Baada ya mashauriano mengi Baruti na Mariam walifunga ndoa. Sherehe ilikuwa ya kifahari kijijini kila mtu alishangilia mwanzo mpya wa familia hiyo lakini ndani ya moyo wa Mariam kulikuwa na maswali mengi ambayo hakuwa na majibu nayo

Ndoa yao ilianza kwa furaha ya kawaida. Baruti alikuwa ni kijana mkarimu na mpole lakini muda ulivyopita katika ndoa yao changamoto ziliibuka polepole. Baruti alikuwa mtu wa kazi sana mara nyingi hakuwa nyumbani na mke wake, Mariam alijikuta akiwa mpweke na watoto wadogo aliowapata ndani ya ndoa hiyo

Anapojaribu kueleza hisia zake kwa Baruti mwanaume huyo hakuwa na wakati wa kumuelewa na alipokuwa akisikitika Baruti, aliona kila kitu kiko sawa huku akijitahidi kupata chakula cha familia na kuendesha maisha ya kawaida

Mariam alikumbwa na upweke na ghafla alihisi kama alikuwa amekwama katika maisha ambayo si yake. Upendo ambao alitarajia haukuja vile alivyofikiria na matarajio ya ndoa kama kisiwa cha amani yalionekana kufifia

Alikumbuka mashairi aliyosoma akiwa mtoto ambapo wanawake waliimba kuhusu ndoa kuwa sehemu ya furaha ya milele lakini sasa Mariam alikuwa na hisia za kutofautisha

“Ndoa sio tu kuhusu kuolewa bali ni kuhusu kupata mpenzi anayekuelewa” Mariam alijitafakari akiwa peke yake usiku huo..

Sehemu inayofuata itakuwa na changamoto mpya za fumbo ambalo linahitaji kufumbuliwa. Fuatilia ili kuelewa

(USIKOSE SEHEMU YA 2) Nunua Simulizi hii Nzuri Ya kusisimua full kwa shilingi 2000 tu.

Nunua hapa👇

Lipia na Thibitisha

Maelekezo ya Malipo:

1. Tuma kiasi Cha 2000TSH kwenda Airtel Money.

2. Hakikisha unatumia namba ya simu: 0695572397 (Jina Lisomeke) JUSTIN BARUTI

3. Hifadhi screenshot ya muamala wako kama uthibitisho.

Thibitisha Malipo Yako

Tags: Riwaya
  • Facebook
  • Twitter
You may like these posts

Post a Comment

Previous Post Next Post
JOEBOY STUDIO

🎉 CHEZA USHINDE ZAWADI 💰

Ad banner

🎰
Cheza
Tuma ujumbe

Follow Us

Popular Posts

Latest

🎬 A NEW LEGEND BEGINS!LEGEND KIDS – THE MOVIE THAT REDEFINES HEROISM!In a world where dreams are tested and courage is rare, Legend Kids introduces us to a new generation of young heroes. 🌟They may be kids—but their spirits are mighty. This film takes you on an unforgettable journey of bravery, friendship, and unstoppable determination. These aren’t your ordinary kids… they’re legends in the making!✨ From the visionary minds behind some of the best youth adventures, Legend Kids is packed with action, laughter, and heartwarming moments that will leave you inspired.🔹 Ordinary kids. Extraordinary dreams. An unforgettable journey.🔹 It’s time for a new generation to rise!📅 Coming soon to theaters near you – PREMIERING on [insert date]!🎟️ Don’t just watch it—feel it.#LegendKidsMovie #NewEraOfHeroes #YoungLegends #InspireTheFuture #MustWatchFilm #ComingSoon

byJOEBOY-July 09, 2025

CHEZA NA USHINDE HADI 50K

July 03, 2025

Habari mteja wangu wa nguvu!Karibu sana kwenye huduma zetu za movie online. Kwa malipo ya huduma, tumia namba yetu rasmi hapa chini:📲 Namba ya Malipo: [43332429](Available kwa WhatsApp & Telegram)NB: Tafadhali hakikisha umetuma ushahidi wa malipo mara baada ya kutuma.Asante kwa kuendelea kutuamini na kufurahia movie kali kila siku!#MovieTime #HudumaBora

July 10, 2025

SUPER QUALITY

May 24, 2025

Main Tags

  • Audio (1)
  • Biashara (1)
  • Chombezo🔞 (2)
  • Latest (1)
  • love story (2)
  • Lovestory (3)
  • lovestory🔞 (2)
  • Movie (11)
  • movies (66)
  • post (2)
  • Riwaya (3)
  • series (4)
  • Simulizi (9)
  • Tangazo (1)
  • Tech (8)
  • Tips (2)

Visitors


JOEBOY STUDIO

JOEBOY STUDIO TABORA

Karibu JOEBOY STUDIO TABORA | Tunajihusisha na huduma za uuzaji movies na Series za aina zote kwa bei nafuu | Pia tunatoa huduma za kutengeneza mabango ya biashara na Logo za biashara kwa gharama nafuu | Pia tunatoa mafunzo ya Computer kwa gharama nafuu Karibuni sana

Design by Theme Developer | Distributed by Blogger Templates
  • Home
  • About Us
  • Contact Us

Contact form